Header Ads

LICHA LIGI KUREJEA WIKIENDI HII, VIGOGO ULAYA JICHO MOJA MECHI ZAO ZA CHAMPIONZ LIGI JUMANNE IJAYO!

UCL-2016-17-1-1
Add caption
BAADA ya Ligi kusimama huko Ulaya kwa Wiki 2 mbili kupisha Mechi za Kimataifa, hasusan zile za kuanza kwa mchujo Makundini kusaka Nchi zitakazocheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia, Ligi hizo tena kilingeni Wikiendi hii lakini Vigogo watacheza huku wakichungulia Mechi zao za UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, za Wiki ijayo.
Mechi hizo za kwanza za Makundi ya UCL zitachezwa Jumanne Septemba 13 na Jumatano Septemba 14.
Siku ya Jumanne mvuto mkubwa ni Mechi za Paris St Germaine na Arsenal ya Kundi A, ile ya Kundi C kati ya Barcelona na Celtic na nyingine ya Kundi C kati ya Man City na Borussia Monchengladbach.             
Jumatano, Mabingwa Watetezi Real Madrid watakuwa kwao Santiago Bernabeu kucheza na jirani zao wa Portugal Sporting Lisbon ambayo pia ndio Klabu aliyoanzia Staa wao Cristiano Ronaldo kabla hajahamia Manchester United.
Mechi nyingine safi za hiyo Jumatano ni zile za Tottenham na AS Monaco huko White Hart Lane Jijini London, Club Brugge na Mabingwa wa England Leicester City wakicheza kwa mara ya kwanza UCL huko Ubelgiji na ile ya Vigogo wa Italy Juventus wakiwa kwao kuivaa Sevilla ya Spain ambao ni Mabingwa wa UEFA EUROPA LIGI kwa Misimu Mitatu iliyopita.

No comments