Header Ads

katika viwanja mbalimbali ambapo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Simba SC ataikaribisha Majimaji ya mjini Songea.

Michuano ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea kesho katika mzunguko wa sita kwa kupigwa michezo mitano katika viwanja mbalimbali ambapo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Simba SC ataikaribisha Majimaji ya mjini Songea.




Afisa Habari wa Simba SC Haji Manara amesema, wanaupa umuhimu mkubwa mchezo huo na hawawezi kuidharau Majimaji kwani kila timu inaingia Uwanjani kwa ajili ya kutafuta pointi tatu.
Kwa upande wake Meneja wa Majimaji Godfrey Mvula amesema, wamejiandaa ili kuhakikisha wanapata pointi tatu kwani wameshapoteza michezo mitano iliyopita hivyo watahakikisha wanapambana kwa ajili ya kujihakikishia ushindi huku wakiahidi kuendeleza ushirikiano na Kocha Kali Ongala ambaye anatarajia kurejea ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kuendelea kukifundisha.
Mechi nyingine zitakazopigwa hapo kesho katika muendelezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ni Mbeya City akiwa ugenini dhidi ya JKT Ruvu katika Uwanja wa Mabatini Mkoani Pwani, Ndanda FC akiikaribisha Azam FC kwa Uwanja wa Nangwanda sijaona Mkoani Mtwara, Tanzania Prisons akiikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya na Mtibwa Sugar akiikaribisha Mbao FC katika Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
Wakati huohuo, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas amevitaka vilabu vya ligi daraja la kwanza vinavyoanza ligi kesho kujifunza kupitia mashindano yaliyopita ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo za kushushwa daraja.

No comments