Msanii wa muziki, Dully Sykes amedai kuwa alipanga kwenda kushoot video ya wimbo ‘Inde’ Afrika Kusini lakini
Msanii wa muziki, Dully Sykes amedai kuwa alipanga kwenda kushoot video ya wimbo ‘Inde’ Afrika Kusini lakini akakwamishwa na muda.
Dully amedai kampuni yake ilikuwa tayari kugharamia baadhi ya gharama za maandalizi ya video hiyo akiwa Afrika Kusini.
“Nilikuwa na bajeti ya kwenda nje lakini kutoka na muda uliisha nikaamua kushoot na Hanscana,” alisema Dully Sykes alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Bajeti ya kwenda nje tulikuwa nayo kwa sababu kuna kampuni inanisimamia. Lakini baada ya kuchelewa akina Harmonize wakaamua kusimamia ile video mpaka ikatoka,”
Video ya wimbo ‘Inde’ inafanya vizuri kwa sasa ambapo kupitia mtandao wa YouTube imeangaliwa mara 1,737,313 kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu.
Post a Comment