Header Ads

Mshambulizi matata wa soka Wayne Rooney, ameachwa nje ya kikosi cha Manchester United cha wachezaji 20



Image copyrightPA
Image captionMshambulizi matata wa Man U Wayne Rooney
Mshambulizi matata wa Man U Wayne Rooney
Mshambulizi matata wa soka Wayne Rooney, ameachwa nje ya kikosi cha Manchester United cha wachezaji 20, watakaosakata mchuano wa Alhamisi wa ligi kuu barani Ulaya mjini Rotterdam dhidi ya timu ya Uholanzi -Feyenoord.
Licha ya kufanya mazoezi siku ya Jumatano, nahodha huyo mwenye umri wa miaka 30 atakosa mechi hiyo ya ufunguzi barani Ulaya.
Wengine ambao wameachwa nje ni pamoja na Luke Shaw, Antonio Valencia na Jesse Lingard.
Maneja wa Manchester United Jose Mourinho, amesema kwamba Rooney amepumzishwa mapema ili kucheza mchuano wa ligi kuu ya Uingereza siku ya Jumapili uwanjani Watford.
Phil Jones pia hayupo baada ya kupata jeraha la goti.
Jeraha hilo litamfanya mlinzi huyo kutocheza kwa muda wa mwezi mmoja hivi.

No comments