Header Ads

KUBAGUANA na kufanya mambo kila mmoja peke yake

 KUBAGUANA na kufanya mambo kila mmoja peke yake, kumetajwa kuwa mwanzo wa chuki na uhasama baina ya wanajamii, wakiwemo wa dini ya Kiislamu.
Image result for PICHA YA MWANAUME PIGA MAZOEZI


Akizungumza wakati wa hotuba ya swala ya Idd el Haj iliyoswaliwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini hapa, Ustadhi Idd Omar Pembe alisema kukosekana kwa umoja na mshikamano ndio chanzo cha kukosekana kwa amani na utulivu.
Ustadhi Pembe alisema Mwenyezi Mungu anawachukia watu wanaobaguana na kufarakana, kwa kuwa kufarakana ni tabia ya shetani inayompeleka mtu motoni.
Awali, akizungumzia dhana ya swala ya Idd el Haj, Imamu wa Msikiti wa Isanga, Shehe Ibrahim Bombo alisema kuwa waumini wa dini ya Kiislamu wanaungana na Waislamu wenzao waliokwenda hija huko Makka, Saudi Arabia.
Shehe Bombo alisema hija ni nguzo ya tano katika nguzo za Uislamu, ambapo Muislamu mwenye uwezo anapaswa kutekeleza ibada hiyo kwa mwaka mara moja katika maisha yake ambapo pia Waislamu wanapaswa kutoa sadaka ya kuchinja mnyama kwa kufuata mwenendo wa Nabii Ibrahimu.
Aliwaonya Waislamu kutofanya maovu siku ya Idd kwa kuwa kufanya hivyo ni sawa na kufanya madhambi siku ya kiama.

No comments