Mchungaji akatisha hotuba ya Trump ya kumpinga Clinton
Mchungaji wa kanisa
moja la watu weusi katika jimbo la Michigan, Marekani amemkatisha
Donald Trump akihutubu alipoanza kumshutumu mpinzani wake Hillary
Clinton.
Mchungaji Faith Green Timmons alimkatisha BwTrump
alipomshutumu mgombea huyo wa chama cha Democratic kuhusu mikataba ya
kibiashara duniani.
"Bw Trump, nilikualika hapa uje kutushukuru
kwa juhudi ambazo tumefanya Flint, si kutoa hotuba ya kisiasa," amesema
pasta huyo wa kanisa la Bethel United Methodist.
"Aha, hilo ni
jambo njema," amemjibu mgombea huyo wa chama cha Republican huku
akionekana kuanza kucheza na karatasi alizokuwa nazo jukwaani.
Bw
Trump ameendelea na kuzungumzia kwa kifupi kuhusu kutatua matatizo ya
maji safi Flint, lakini baadhi ya watu kwenye umati wakaanza kumzomea.
Mwanamke mmoja amesema kwa sauti kwamba mfanyabiashara huyo tajiri alitumia njia za kibaguzi katika majumba yake.
Mfanyabiashara huyo amejibu: "Haiwezekani, umekosea. Singeweza kufanya hivyo."
Mchungaji
huyo ameingia tena na kuwashutumu waliokuwa wanamzomea Bw Trump na
kusema: "Yeye ni mgeni katika kanisa langu na mtamheshimu".
Bw Trump mwishowe amelazimika kukatiza ghafla hotuba yake, ambayo imedumu kwa dakika sita hivi.
Post a Comment