Header Ads

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amerudisha pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba yake binafasi



Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amerudisha pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba yake binafasi jinsi ilivyoamriswa na mahakama.
 Pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba ya Zuma zilikuwa ni za mlipa kodi



Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anaripoti kuwa msemaji wa wizara ya fedha amethibitisha kuwa pesa hizo zimepokelewa.
Wizara ya fedha nchini Afrika Kusini ilikuwa imependekeza kuwa Rais Zuma alihitajika kurejesha dola 509,000 kwa serikali, pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba yake huko Nkandla.
Image copyright AFP
Image caption Makao ya binafsi ya Zuma ya Nkandla
Mahakama ya juu zaidi nchini humo ilikuwa imetoa uamuzi mapema mwaka huu, kuwa Zuma alipe dola milioni 23 pesa za umma zizotumiwa kwa nyumba yake mwaka 2009.
Sakata ya Nkandla ilitishia wadhifa wake Zuma. Alikwepa hatua ya kumuondoa madarakani na shinikizo za kumtaka ajiuzulu.
Hata hivyo aliomba msamaha kwa njia ya runinga mwezi Aprili akisema kuwa suala hilo limeleta aibu.

No comments