Jose Mourinho amesema kwamba atarejelea kikosi cha kawaida cha klabu hiyo wakati wa mechi dhidi ya Watford
Meneja wa Manchester Unitedbaada ya kushindwa na Feyenoord mechi ya Europa League Alhamisi.
Mourinho alifanya mabadiliko manane kwenye kikosi kilichocheza mechi ya Alhamisi ambapo walicheza vibaya na kulazwa 1-0. Bao lilifungwa na Tonny Vilhena dakika ya 79.
Mechi hiyo ilikuwa ya nne kwa Man Utd kushindwa ugenini Ulaya na ilijiri siku tano tu baada yao kushindwa debi na Manchester City 2-1 Jumapili.
Nahodha Wayne Rooney na wakabaji Antonio Valencia na Luke Shaw walipumzishwa kwa ajili ya mechi hiyo ya Ligi ya Premia itakayochezwa Jumapili saa nane saa za Afrika Mashariki.
Nafasi ya Valencia aliwekwa Matteo Darmian naye Marcos Rojo akajaza nafasi ya Shaw.
Ander Herrera, Anthony Martial, Juan Mata, Marcus Rashford, Morgan Schneiderlin na Chris Smalling walikuwa wachezaji hao wengine walioingizwa kikosini mechi hiyo iliyochezewa uwanja wa De Kuip.
Mourinho amesema: "Tunarejelea kikosi cha kawaida bila mabadiliko makubwa."
Paul Pogba alikuwepo safu ya kati lakini hakuweza kutamba.
"Huwa sitaki kuangalia wachezaji binafsi sana," amesema Mourinho . "Ni jambo nisilopenda."
"Nafikiri ni kama alicheza kama timu yote. Kipindi cha kwanza walidhiti mechi lakini kasi yao ilikuwa nusu. Kipindi cha pili waliongeza kasi na hapo ndipo tulifungwa
Post a Comment