Header Ads

Vikosi vya ulinzi na usalama vimefungua mafunzo ya pamoja ya utendaji kivita kwenye maeneo ya fukwe na visiwa

Vikosi vya ulinzi na usalama vimefungua mafunzo ya pamoja ya utendaji kivita kwenye maeneo ya fukwe na visiwa vilivyopo ndani ya bahari kwa lengo la kukabiliana na maovu yatendekayo ndani ya bahari na kuimarisha ulinzi.


Mafunzo hayo ya pamoja ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ yameshirikisha vikosi vya Anga, Nchini Kavu na Baharini, JKT na Wanamgambo kwa lengo la kuwajengea uwezo kivita na huku ikielezwa kuwa Jeshi la Tanzania ni miongoni mwa majeshi bora dunia.
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Venance Mabeyo amesema jeshi limekuwa imara katika kuhakikisha linakabiliana na vitendo vya uharamia, ugaidi, uvuvi haramu na uingizwaji wa madawa ya kulevya na uhalifu wowote unaoweza kutokana na fukwe zetu.

Mafunzo hayo yatahitimishwa Wilayani Bagamoyo Septemba 30 na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli huku Kaimu Mkuu wa Kamandi ya Wanamaji akiwataka watanzania kutambua kuwa Jeshi lao lipo imara katika kulinda mipaka yao.

No comments