Kamati ya maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imetangaza hukumu dhidi ya vituo viwili vya Redio vilivyofungiwa
Kamati ya maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imetangaza hukumu dhidi ya vituo viwili vya Redio vilivyofungiwa kutokana na kile serikali ya nchi hiyo ilichosema kuwa ni kuchochea ghasia na kumkashifu Rais John Magufuli.
Vituo vilivyokuwa vimefungiwa kwa muda usiojulikana kwa tuhuma za kukiuka Sheria za Utangazaji ni Magic FM cha jijini Dar es Salaam na Redio 5 cha jijini Arusha kaskazini mwa Tanzania.
Kupitia maamuzi yaliyosomwa na Makamu mwenyekiti wa kamati ya maudhui Joseph Mapunda Kamati imeikuta Redio 5 na hatia ya kumkashifu rais na kuchochea uvunjifu wa amani na hivyo imehukumiwa kulipa shilingi milioni 5 za Tanzania sawa na takribani dola 2,200 za Marekani.
Aidha, kituo hicho cha redio kimefungiwa kutorusha matangazo kwa miezi mitatu na kuwekwa chini ya uangalizi wa mwaka mmoja.
Wakati huo huo Radio Magic FM imepewa onyo na kutakiwa kumwomba radhi rais wa Tanzania pamoja na wasikilizaji wa redio hiyo kwa siku tatu mfululizo.
Tangu tarehe 29 mwezi Agosti 2016 Waziri wa Habari nchini humo Nape Nnauye alitangaza kuvifungia vituo hivyo viwili vya redio kwa muda usiojulikana kwa madai kuwa vilikiuka sheria za utangazaji.
Hukumu hiyo iliiibua minong'ono miongoni mwa wananchi wa Tanzania wakidai kuwa huo ni uminyaji wa uhuru wa habari hasa katika kipindi ambacho Tanzania iko katika vuguvugu kali la mvutano kati ya Serikali na vyama vya upinzan
chazo bbc
Post a Comment