Header Ads

Waendesha mashtaka nchini Marekani wamemfungulia mashtaka Ahmad Khan Ramani kwa kutega mabomu huko New York

Waendesha mashtaka nchini Marekani wamemfungulia mashtaka Ahmad Khan Ramani kwa kutega mabomu huko New York


Ahmad Khan RahamiImage copyrightREUTERS
Image captionAhmad Khan Rahami alijeruhiwa wakati wa kukamatwa
Waendesha mashtaka nchini Marekani wamemfungulia mashtaka Ahmad Khan Ramani kwa kutega mabomu huko New York na New Jersey mwishoni mwa wiki ambapo mlipuko mmoja ulijeruhi watu 31.
Waendesha mashtaka wanasema kuwa Bw Rahami ambaye ni mhamiaji kutoka Afghanistan, alinunua vifaa na vitu vya kuunda bomu kupitia kwa mtandao na kuandika makala akilisifu kundi la Islamic State.
Ulinzi umeendelea kuimarishwa jijini New YorkImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionUlinzi umeendelea kuimarishwa jijini New York
Pia ameshtakiwa kwa kujaribu kuwaua polisi wakati akikamatwa siku ya Jumatatu.
Shirika la ujasusi la marekani FBI linasema kwa lilimchunguza Rahami mwaka 2014 lakini halikumpata na chochote cha kumhusisha na ugaidi wakati huo.
Watu 29 walijeruhiwa kwenye mlipuko uliotokea mtaa wa Chelsea, New York. Kilipuzi ambacho hakikuwa kimelipuka kilipatikana hapo karibu.
Vilipuzi vingine kadha vilikuwa vimepatikana New Jersey siku za hivi karibuni.
Tuyajuayo kufikia sasa:
  • Ahmad Kham Rahami alikamatwa kuhusiana na milipuko ya New York na New Jersey
  • Ni raia wa Marekani mzaliwa wa Afghanistan
  • Anakabiliwa na mashtaka matano ya kujaribu kuwaua maafisa wa polisi, lakini hakuna mashtaka yoyote yanayohusiana na ulipuaji kufikia sasa
  • Anakabiliwa pia na mashtaka ya kutega mabomu New York na New Jersey
  • Waendesha mashtaka wanasema aliandika makala akilisifu kundi linalojiita Islamic State

No comments