Header Ads

Rais MAGUFULI amepokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola Laki Mbili za Kimarekani sawa na Shilingi Milioni MIA NNE

 Rais MAGUFULI amepokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola Laki Mbili za Kimarekani sawa na Shilingi Milioni MIA NNE 


Rais Dokta JOHN MAGUFULI amepokea taarifa ya maafa yaliyosababishwa na tetemoko la ardhi lililotokea katika Mkoa wa KAGERA na mikoa jirani ya MWANZA, GEITA na MARA kutoka kwa Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA, Ikulu Jijini DSM.

Pamoja na kupokea taarifa hiyo Rais MAGUFULI amepokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola Laki Mbili za Kimarekani sawa na Shilingi Milioni MIA NNE na Therathini na Saba kutoka kwa Rais YOWERI MUSEVENI wa UGANDA

Rais MAGUFULI pia amepokea taarifa ya mchango wa mabati, mablanketi na magodoro vyenye thamani ya Shilingi Milioni 115 kutoka kwa Rais UHURU KENYATTA wa KENYA kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani KAGERA na kuwaomba wananchi wafanye kazi huku misaada hiyo ikiendelea kuwafikia.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya maafa na michango kwa ajili ya waathirika wa maafa hayo, Rais MAGUFULI amewashukuru wote waliojitoa kusaidia waathirika wakiwemo Marais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais UHURU KENYATTA wa KENYA na PAUL KAGAME wa R
WANDA ambao wamempigia simu za kumpa pole na tayari wametoa misaada yao.

Rais MAGUFULI pia amezishukuru nchi mbalimbali, mashirika, wafanyabiashara, watumishi wa umma na watu binafsi kwa misaada yao na kusema michango hiyo ina umuhimu mkubwa katika kukabiliana na athari za maafa hayo.

No comments