SIMBA jana iliendeleza ubabe kwa Mtibwa Sugar baada ya kuifunga mabao 2-0
SIMBA jana iliendeleza ubabe kwa Mtibwa Sugar baada ya kuifunga mabao
2-0 katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es
Salaam.
Mechi hiyo iliyokuwa ikitarajiwa kuwa ya vuta nikuvute, Simba
ilionekana kutawala mchezo katika vipindi vyote viwili. Ushindi huo
unaifanya Simba kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ikifikisha
pointi 10 sawa na Azam katika mechi nne ilizocheza, ikishinda tatu na
kutoka sare moja.
Iliichukua Simba dakika 52 kuandika bao la kuongoza katika mechi hiyo
likifungwa na Ibrahim Ajib aliyefunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa
kona uliopigwa na Mohamed Hussein, ‘Zimbwe Jr’.
Bao hilo lilizidi kuamsha safu ya ushambuliaji ya Simba ambayo
ilikuwa ikilishambulia lango la Mtibwa Sugar kama nyuki ambapo dakika ya
66 ilipata bao la pili lililofungwa na Mrundi Laudit Mavugo.
Mavugo alifunga bao hilo kwa kazi nzuri iliyofanywa na Mwinyi
Kazimoto aliyeambaa na mpira nje ya 18 kabla ya kuachia shuti maridadi
lililomkuta Mavugo ambaye hakufanya ajizi akaujaza mpira wavuni.
Mtibwa katika mechi ya jana itabidi ijilaumu kwani pamoja na kubanwa
na safu ya ulinzi ya Simba lakini ilipata nafasi kadhaa ikashindwa
kuzitumia hasa ile ya dakika ya 16 pale Haruma Chanongo alipounganisha
pasi ya Stahmili Mbonde lakini shuti lake liliokolewa na mabeki wa
Simba.
Chanongo alikosa bao lingine katika dakika ya 32 kwa pasi ya Mbonde
lakini alip
aisha akiwa peke yake na kipa wa Simba Vincent Angban.
Kikosi cha Simba SC: Vincent Angban, Janvier Bokungu, Mohammed
Hussein ‘Zimbwe Jr’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza
Kichuya/Frederick Blagnon, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Ibrahim
Hajib/Jamal Mnyate, Mwinyi Kazimoto/Said Ndemla.
Mtibwa Sugar: Abdallah Makangana, Ally Shomary, Issa Rashid, Cassian
Ponera, Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Kevin Friday/Mohammed Juma, Ally
Yussuf, Stahmili Mbonde, Ibrahim Juma/Hussein Javu, Haroun Chanong
Post a Comment