Kocha wa timu ya Manchester United amesema wachezaji wake walicheza bila malengo
Kocha wa timu ya Manchester United Jose Mourinho
Kocha wa timu ya Manchester United amesema wachezaji wake walicheza bila malengo ya kupata ushindi kwenye mchezo wao wa jana dhidi ya Feyenoord ya UHOLANZI wa michuano ya EUROPA.
Katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi Manchester United ilifungwa bao moja kwa bila, goli lilotiwa kimiani na Tonny Vilhena katika dakika ya 79 ya mchezo.
Kocha huyo MRENO na mwenye maneno mengi amesema timu yake haukucheza vibaya hasa kwenye kipindi cha kwanza na mchezo huo ila ukosefu wa malengo na mbinu kwa wachezaji wake kulifanya MANCHESTER UNITED kupoteza mchezo huo.
MOURINHO akaongeza kwa kusema wachezaji wake hawakupambana ili kushinda mchezo huo bali walicheza ili kuonyesha uweo wa kumili mpira basi.
Katika kikosi kilichocheza jana MOURINHO alifanya mabadiliko ya wachezaji nane na mwenyewe anatetea uamuzi huo kwa kusema timu hiyo ilikuwa imara na ingeweza kuibuka na ushindi.
Post a Comment