Header Ads

Zaidi ya watu 130 wanaripotiwa kufariki dunia na wengine 400 hawajuilikani walipo nchini Korea


Zaidi ya watu 130 wanaripotiwa kufariki dunia na wengine 400 hawajuilikani walipo nchini Korea Kaskazini kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga Lion-rock.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mafuriko hayo yamelikumba eneo la Kaskazini Mashariki mwa Mto Tumen, linalopakana na China, ambapo maelfu ya watu wamepoteza makaazi yao.

Kuna ripoti za majengo na miundombinu muhimu kuharibiwa kabisa.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kiutu-OCHA, imesema  watu wapatao 140,000 wana mahitaji makubwa ya msaada, miongoni mwao 100,000 hawana makaazi.

September 13, 2016

No comments