Umoja wa Mataifa unasema kuwa idadi ya watu waliokimbia nchi ya Sudan Kusini
Umoja wa Mataifa unasema kuwa idadi ya watu waliokimbia nchi ya Sudan Kusini kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo imepita watu milioni moja.
Idadi hiyo inajumuisha zaidi ya watu 185,000 ambao wameikimbia nchi kufuatia mapigano mapya yaliyoanza mwezi Julai.
Zaidi ya watu milioni 1.6 nao wamelazimika kuhama makwao ndani ya Sudan Kusini.
Makadirio ya idadi ya watu nchini Sudan Kusini ni kati ya watu milioni 10 hadi milioni 12. Hii inamaaanisha kuwa takriban asilimia 20 ya watu hao hawana makao kutokana na mzozo uliopo.
Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalizuka mwezi Disemba mwaka 2013 na kundlea hadi sasa, licha ya kuwepo mkataba wa amani uliotiwa sahihi mwaka uliopita.
Post a Comment