Header Ads

ndege kuangukia nyumba mjini Phoenix, Arizona.

ndege  kuangukia nyumba  mjini Phoenix, Arizona.
 Ndege yaangukia nyumba nchini Marekani
Rubani ,pamoja na warukaji wa 4 wa angani pamoja pia  wakaazi wawili wa nyumba wamenusurika kifo baada ya ndege moja kuanguka katika nyumba moja mjini Phoenix, Arizona.
Maafisa wa kukabiliana na moto katika makaazi ya Gilbert wanasema watu waliokuwepo katika ndege hiyo waliweza kutoka ndani ya ndege hiyo kabla ya kunagukia nyumba hiyo.
Kulikuwa na watu wawili ndani ya nyumba hiyo ,lakini hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa.
Rubani wa ndege hiyo alipelekwa hospitalini na kutibiwa majeraha madogo madogo ya moto kulingana na polisi.
Hakuna mrukaji wa angani aleyeumia .Inadaiwa kwamba ndege hiyo ilikuwa ikibeba warukaji wa angani kwa sherehe ya katiba,siku inayoadhimishwa kila mwaka kusherehekea katiba ya Marekani.

No comments