Header Ads

WATU 16 MBALONI NCHINI CONGO

WATU 16 MBALONI  NCHINI  CONGO


Wafuasi wa upinzani wakifanya maandamano nchini DRC
Umoja wa Mataifa unasetangaza kuwa wakereketwa wa demokrasia 16 wametiwa mbaroni katika Jamhuri wa Demokrasia ya Congo.
Umoja wa Mataifa umehimiza taifa hilo kuheshimu haki za kimsingi za kibinadamu nchini humo.
Umoja wa Mataifa pia unasema kuwa watu wengine 85 wametiwa mbaroni katika mji mkuu wa Lubumbashi, baada ya makabiliano makali kati ya maafisa wa usalama na wafuasi wa vyama vya upinzani mnamo Ijumaa.
Hakukuwa na tamko lolote kuhusiana na hatua hiyo kutoka kwa serikali.
Uchaguzi unatarajiwa mnamo Novemba, lakini tume ya uchaguzi inasema kuwa uchaguzi huo utacheleweshwa.
Upande wa upinzani unamlaumu rais Joseph Kabila, ambaye haruhusiwi kikatiba kugombea kiti hicho tena, kwa kuchelewesha uchaguzi huo makusudi.

No comments