Sergio Aguero amefunga 'hat-trick' yake ya pili msimu huu na kuwawezesha Manchester City kupata ushindi
Kwenye mechi hiyo ya kwanza hatua ya makundi
Ulaya chini ya Pep Guardiola, Aguero alifunga baada ya kupokea krosi
kutoka kwa Aleksandar Kolarov kisha akafunga penalti baada ya Ilkay
Gundogan kuchezewa visivyo na kufanya mambo kuwa 2-0 wakati wa mapumziko
Baadaye alimchenga kipa na kufunga bao kwenye lango wazi dakika ya 77.
Mechi hiyo ilitazamwa na mashabiki 32,000, baada ya kuahirishwa kutoka Jumanne kutokana na mvua.
Nguvu mpya Kelechi Iheanacho alikamilisha ufungaji dakika za mwisho mwisho.
Sergio Aguero, 28, sasa amefunga mabao 25 Ligi ya Mabingwa, moja zaidi ya nyota wa zamani wa Manchester United Paul Scholes.
Aguero
atakosa mechi ya Jumamosi Ligi ya Premia dhidi ya Bournemouth na mechi
ya Kombe la Ligi ugenini Swansea kutokana na marufuku ya mechi tatu
anayoendelea kuitumikia.
City watarejea tena kucheza Ligi ya Klabu Bingwa
Ulaya tarehe 28 Septemba ugenini kwa Celtic, waliochapwa 7-0 na
Barcelona Jumanne.
Post a Comment