Header Ads

Ligi kuu TANZANIA BARA inaingia kwenye raundi


 Ligi kuu TANZANIA BARA inaingia kwenye raundi ya tano hapo kwa kesho JUMAMOSI ambapo kutachezwa michezo SITA na kesho kutwa JUMAPILI kutakuwa na mchezo mmoja utakaochezwa kwenye dimba la KAMBARAGE huko SHINYANGA.

Kwenye raundi hiyo ya TANO kutakuwa na michezo miwili ya wapinzani wa mjii mmoja yaani CITY DEBY,  jijini DSM, vinara wa ligi hiyo AZAM FC watakipiga na SIMBA kwenye dimba la UHURU na huko MBEYA , wagonga nyundo wa JIJI hilo la kijani MBEYA CITY watacheza na wapinzani wao wa jadi TANZANIA PRISONS.

Akizungumzia mchezo dhidi ya AZAM FC msemaji wa SIMBA, HAJI MANARA amesema wao hawana wasiwasi na kuhusu wakacheze wapi mchezo huo alisema popote wao wapotayari kucheza.

`` sisi kama SIMBA tunaangalia mchezo wenyewe na umuhimu wake na hatuangali utachezwa wapi`` alisema MANARA.

Kwa upande wake kocha wa timu ya TANZANIA PRISONS ABDUL MINGANGE ameimbia TBC mchezo dhidi ya MBEYA CITY siku zote unakuwa mgumu.

`` kucheza na MBEYA CITY siku mchezo unakuwa na presha sana kwasababu hawa ni wapinzani wetu wa jadi ila sisi tumejianda vya kutosha na malengo yetu ni kupata ushindi``. Alisema MINGANGE.

Mkoani SHINYANGA kwenye dimba la KAMBARAGE mabingwa watetezi YANGA watakuwa wageni wa MWADUI FC,wakati wanajeshi wa jeshi la kujenga TAIFA, RUVU SHOOTING wao watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa MABATINI kucheza na MBAO FC ya MWANZA.
MTIBWA SUGAR itacheza na KAGERA SUGAR na MAJI MAJI ya SONGEA inayoburuza mkia hadi sasa itakuwa nyumbani kucheza na wanachele NDANDA FC ya MTWARA.

JUMAPILI tarehe 18 septemba chama la wana, STAND UNITED itacheza na JKT RUVU huko mkoani SHINYANGA.

Hadi sasa AZAM FC inaongoza kwenye msimamo wa ligi hiyo pamoja na SIMBA zote zikiwa na pointi kumi huku wakizidiana kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufunga wakifuatiwa na mabingwa watetezi YANGA wenye pointi saba sawa na timu zingine tatu za MBEYA CITY, RUVU SHOOTING na TANZANIA PRISONS zote zikiwa na pointi sana zikizidiana magoli ya kufunga na kufungwa.

No comments