Mkuu wa Magereza nchini Jenerali JOHN MINJA amezuia kupandishwa vyeo kwa askari kadhaa wa jeshi la Magereza
Mkuu wa Magereza nchini Jenerali JOHN MINJA amezuia kupandishwa vyeo kwa askari kadhaa wa jeshi la Magereza
Mkuu wa Magereza nchini Jenerali JOHN MINJA amezuia kupandishwa vyeo kwa askari kadhaa wa jeshi la Magereza ambao wamehitimu mafunzo yao katika chuo cha KIWIRA wilayani RUNGWE mkoani MBEYA.
Jenerali MINJA ametangaza uamuzi huo baada ya kubainika kuwepo kwa kasoro kadhaa miongoni mwa askari hao ambazo ni pamoja na utoro na kushindwa kufuatilia kikamilifu mafunzo ya uongozi daraja la Kwanza.
Mkuu huyo wa Jeshi la Magereza Nchini ametangaza uamuzi huo wakati wa kufunga mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kozi namba 22 kwa wahitimu ya 680 katika chuo cha Magereza KIWIRA.
Jenerali MINJA pia ametangaza utaratibu mpya wa upandishwaji wa yeo kwa askari wa jeshi la magereza, baada ya kubainika kuwa baadhi ya askari hao wamekuwa wakitoroka mafunzo.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani na nchi Meja Jenerali PROJEST RWEGASIRA amewataka askari wa jeshi la mageraza nchini kuheshimu misingi ya kazi yao.
Post a Comment