Header Ads

Kamati ya Maafa ya mkoa wa KAGERA imeanza kutoa misaada kwa waathiriwa wa tetemeko


Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu Akiongoza Zoezi la Kugawa Mahitaji kwa Waathirika wa tetemeko la ardhi la Kagera
Kamati ya Maafa ya mkoa wa KAGERA imeanza kutoa misaada kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10 mwaka huu mkoani KAGERA na kusababisha vifo vya watu 17 na kuacha nyumba zaidi ya elfu moja zikiwa katika hali mbaya.

Wakizungumza mara baada ya kupokea misaada waathiriwa hao wameishukuru serikali kwa misaada hiyo na kusema kwa sasa baadhi yao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mahema katika makazi yao ya muda.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa KAGERA Meja Jenerali Mstaafu SALUM KIJUU ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati ya maafa ya mkoa amewahakikishia waathiriwa hao kuwa serikali iko nao bega kwa bega katika kuhakikisha wanapata misaada yote inayotolewa.

Kamati ya maafa ya mkoa wa KAGERA inaendelea kupokea misaada mbalimbali na kuigawa kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi lililotokea Jumamosi iliyopita.

No comments