Header Ads

J .I AJA NA SONG Shengelee

Kidato Kimoja ulikuwa wimbo uliopendwa na kila rika na ulimweka J.I kwenye kilele cha mafanikio.

13687067_315611228790848_6839169_n
Mwaka jana aliachia wimbo uitwao ‘Msifie Wife’ anaokiri kuwa haukupata muda wa hewani vya kutosha. Na sasa amekuja na wimbo mpya uitwao ‘Shengelee’ wenye kila dalili za kumrejesha tena kwenye playlist za redio na TV nyingi.
Akiongea na Bongo5, muimbaji huyo amesema wingi wa wasanii umefanya kuwe na changamoto kwa nyimbo kupenya.
“Zamani tulikuwa wasanii kwanza wachache sana na muziki haukuwa bado na biashara kubwa kama ulivyo sasa hivi,” J.I ameiambia Bongo5.
13687067_315611228790848_6839169_n
“Kwahiyo sasa hivi wasanii tumekuwa wengi muziki umekuwa biashara kubwa sana kwahiyo kuna challenge nyingi, kila mtu anataka kufanya sanaa.”
“Lakini kwasababu naamini nina uwezo na nafanya kazi ambazo zina viwango vya juu nina imani tutakwenda sawa,” amesisitiza.


No comments