Header Ads

NAIBU Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo amenusurikia kifo






NAIBU Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo amenusurikia kifo baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kugongana na gari lingine katika eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya leo.


Ajali hiyo imehusisha gari dogo aina Toyota Corola iliyokuwa ikotokea Mbeya kwenda Rungwe na Naibu Waziri Selemani Jafo alikuwa akitokea Tukuyu kikazi.
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema katika gari la Naibu Waziri kulikuwa na watu watatu, Waziri Jafo mwenyewe, Katibu wake na Dereva na wote walitoka salama katila ajali hiyo.
Amesema baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya uchunguzi kuona kama wameumia au laa.
Mtunguja amesema baada ya uchunguzi Waziri na wenzake waliendelea na safari yao kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahi vikao vya Bunge, vinavyotarajia kuanza kesho.

No comments