Header Ads

Safari ya miezi saba ya bajaji inayotumia kawi ya jua na nguvu za umeme

KALI ZOTE BLOG

Naveen RabelliImage copyrightNAVEEN RABELLI
Image captionBw Rabelli alifanyia ukarabati bajaji ya dizeli kuiwezesha kutumia umeme na kawi ya jua
Safari ya miezi saba ya bajaji inayotumia kawi ya jua na nguvu za umeme, ambayo ilikuwa inatoka India kwenda hadi Uingereza, imesitishwa kwa muda baada ya wezi kuiba hati ya kusafiria ya dereva wa gari hilo karibu na mji wa Paris.
Mhandisi Naveen Rabelli aliibiwa pasipoti na pochi yake eneo la Sarcelles, alipokuwa ameenda haja.
Kwa sasa anasubiri kupata pasipoti mpya ndipo aweze kuvuka English Channel na kuhitimishia safari yake katika Kasri la Buckingham.
Bw Rabelli anajaribu kuwahamaisha watu kutumia kawi mbadala.
"Nimekuwa safarini kwa miezi saba sasa, na nimekuwa na hamu kubwa ya kufika Uingereza. Nimejiandaa kwa hili kwa miaka minne," ameambia BBC.
"Inaniuma sana kupoteza pasipoti yangu na euro 1,000" nikiwa safarini kuelekea Calais ambapo ningeabiri feri na kuingia Uingereza, amesema.
Naveen RabelliImage copyrightNAVEEN RABELLI
Image captionBw Rabelli akiwa na walinzi wa mpakani
Naveen RabelliImage copyrightNAVEEN RABELLI
Image captionBajaji yake 'ilitakaswa' kabla yake kuanza safari India
Bw Rabelli amesaidiwa na Wasamaria wema safarini.
Amepitia Iran, Uturuki, Ugiriki, Bulgaria, Serbia, Austria, Ujerumani na Uswizi.
Huwa analala kwenye bajaji hiyo anapokosa mtu wa kumpa malazi.
Amefanikiwa kuweka akipa pesa nyingi kwa njia hii.
Mwanamume huyo wa miaka 35 ni mkazi wa India lakini ni raia wa Australia na amekuwa akifanyia kazi kampuni ya kuunda magari ya kutumia umeme nchini India, Mahindra Reva.
Alinunua bajaji hiyo $1,500 (£1,120) na akatumia $11,500 kuifanyia ukarabati.
Kwa sasa, bajaji yake inaweza kufikia kasi ya juu ya 60km/h (37 mph) ana hutumia umeme na kawi ya jua.
Gari hilo lake lina kitanda na jiko la sola.
Tuk-tukImage copyrightNAVEEN RABELLI
Image captionSafari hiyo ni ya umbali wa 14,500km
Naveen RabelliImage copyrightNAVEEN RABELLI
Image captionAkiwa na marafiki Abhar, Iran
Naveen RabelliImage copyrightNAVEEN RABELLI
Image captionAiwa nje ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Alexander Nevski mjini Sofia, Bulgaria

No comments