Header Ads

Hali ya wasiwasi wa usalama imetanda katika mji mkuu wa Gabon




KALI ZOTE BLOG


Image result for picha ya BUNDUKI






Hali ya wasiwasi wa usalama imetanda katika mji mkuu wa Gabon, Libreville kufuatia vurugu zilizoibuka baada ya uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki na hivyo kusababisha vikosi vya usalama kusambazwa katika mji huo. 

Vurugu ziliibuka Jumatano wiki hii baada ya tume ya uchaguzi nchini humo kumtangaza Rais Ali Bongo kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais. Hadi sasa watu watano wameripotiwa kuuawa kutokana na vurugu hizo huku baadhi ya raia wakitaka kurejea kwa utulivu



 nchini humo. Ali Bongo alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa rais wa nchi hiyo mwaka 2009 kufuatia kifo cha baba yake, Omari Bongo ambaye alilitawala taifa hilo kwa muda wa miaka 42. Kiongozi wa upinzani aliyeshindana na Rais Bongo katika kinyang'anyiro hicho, Jean Ping ambaye amejitangaza mshindi, amesema uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu na ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati.


SORCE DW

No comments