Header Ads

Rais wa Marekani, Barack Obama anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uingereza

Rais wa Marekani, Barack Obama anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uingereza, Therasa May hii leo pembezoni mwa mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi zenye uchumi mkubwa duniani-G20 nchini China. 




Image result for picha ya obama



Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa viongozi hao kukutana rasmi tangu May ashike madaraka hayo mwezi Julai kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu David Cameron baada ya Waingereza kupiga kura ya maoni kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya

. Rais Obama aliwatahadharisha Waingereza kutopiga kura ya kujiondoa kwenye umoja huo akisema hatua hiyo inaweza kurejesha nyuma mahusiano ya kibiashara kati ya Marekani na taifa hilo. Viongozi hao wanatarajiwa kujadili masuala mbalimbali yahusuyo mahusiano kati ya nchi hizo mbili pamoja na masuala mengine ya kidunia.


 Obama anatarajiwa pia kuwa na mazungumzo na Rais wa China, Xi Jimping wakati wa mkutano huo wa kilele wa G20 na baadaye kukutana na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, wakati ambapo mahusiano kati ya nchi hizo mbili yakionekana kuingia dosari kufuatia hatua ya Uturuki kujiingiza kijeshi katika mgogoro wa Syria.

No comments