Jackie Chan kukabidhiwa tuzo ya heshima
KALI ZOTE BLOG
Muigizaji wa filamu za Hollywood, Jackie Chan anatarajiwa kupokea tuzo ya kujitolea ya Oscar kutokana na mchango wake kwenye tasnia ya filamu.
Wengine wanaotarajiwa kupewa tuzo kama hiyo kwa mchango wao kwenye filamu ni pamoja na mhariri wa filamu za Uingereza, Anne V. Coates, muongozaji wa filamu Lynn Stalmaster na muandishi wa makala Frederick Wiseman.
Rais wa jopo lililohusika kuwateuwa watu hao, Cheryl Boone Isaacs amewataja watu hao kama ni waasisi halisi kwenye tasnia hiyo ya filamu.
“True pioneers and legends in their crafts,” amesema Cheryl. Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika mwezi Novemba, mwaka huu huko Los Angeles.
Mwaka 2016 umekuwa wa neema kwa muigizaji huyo kutokana na hivi karibuni kuorodheshwa kwenye jarida la Forbes kama muigizaji anayeshika namba mbili kwa kulipwa zaidi kwenye filamu akiwa anaingiza kiasi cha $61m
Post a Comment