Mkubwa Fella aonyesha nyumba 4
Mkurugenzi wa Yamoto Band, Mkubwa Fella ameonyesha nyumba nne za wasanii wake wa Yamoto Band baada ya baadhi ya watu kuhoji kuhusu mafanikio ya wasanii hao.
Nyumba nne za wasanii hao
Akiongea naKALI ZOTE BLOG Ijumaa hii akiwa Mbande Kisewe, Chamazi jijini Dar es salaam, Fella amesema ameamua kuonyesha nyumba hizo baada ya kuchoka maswali ya watu kuhusu mafanikio ya wasanii hao.
Fella akizunguza na waandishi wa habari
“Leo nimewaita hapa Mbande Kisewe siyo kuzindua ila kuwaonyesha kwa sababu kuna meseji nyingi nazipata, Mkubwa vipi mbona watoto wananenepa wanavaa vizuri, maendeleo vipi, mbona kuna wasanii wamekuja juzi tu, tunawaona wanafanya vitu vikubwa. Kwa hiyo nimewajengea hizi nyumba lakini bado hazijazinduliwa, nataka uzinduzi wake Mh rais mtaafu Kikwete aje azindue na kuwakabidhi hawa vijana nyumba zao,” alisema Fella.
Aliongeza, “Kwa hiyo nataka wale wanaosema Yamoto wananini waone nini kimefanyika, kwa sababu nilikuwa natengeneza kitu kikubwa, siyo vibanda majumba na mlivyoyaona. Kwa hiyo 80% nyumba zimekamika, kuna vitu ambavyo sijamalizia kwa sababu kila mtu najua atataka kuweka manjonjo yake kwenye nyumba yake, kwa hiyo ndani ya miaka mitatu tulichovuna tumekiwekeza kwenye hizi nyumba, ni kubwa naza kisasa kabisa,”
Meneja huyo siyo mara yake ya kwanza kuwajengea wasanii wake nyumba, alishafanya hivyo kwa Temba na Chege pamoja Juma Nature. Angalia picha.
Fella akiwa na Temba
Moja kati ya nyumba za wasanii wa Yamoto Band
Mwonekano wa wa nyumba
Post a Comment