Header Ads

LIGI Kuu ya soka ya wanawake inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 4

LIGI Kuu ya soka ya wanawake inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 4 mwaka huu. Hii ni mara ya kwanza kufanyika ligi ya wanawake nchini.




Mwaka jana ilifanyika michuano ya kombe la taifa la wanawake kwa mara ya kwanza ambapo ilishirikisha mikoa yote ya Tanzania Bara na Temeke kuibuka mabingwa.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Wanawake Tanzania (TWFA) Amina Karuma alisema ligi hiyo itashirikisha timu 12 zitakazogawanywa katika makundi mawili yenye timu sita sita kila moja.
“Tutakuwa na kundi A na kundi B ambapo zitacheza mechi nyumbani na ugenini kisha timu tatu za juu kutoka kila kundi zitacheza ligi ya mkondo mmoja na kumpata bingwa,” alisema.
Timu zinazotarajiwa kushiriki ligi hiyo ni Viva Queens ya Mtwara, Fair Play FC ya Tanga, Panama FC ya Iringa, Mlandizi Queens ya Pwani, Marsh Academy ya Mwanza, Baobao Queens ya Dodoma, Majengo Queens ya Singida, Kigoma Sisters FC ya Kigoma, Kagera Queens ya Kagera, JKT Queens, Mburahati Queens na Evergreen Queens za Dar es Salaam.
Aidha kuelekea kwenye ligi hiyo iliyodhaminiwa na Azam, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeandaa semina elekezi kwa timu shiriki. Taarifa ya TFF ilisema semina hiyo itafanyika kesho kwenye Ukumbi wa Hosteli za TFF zilizopo ofisi za Makao Makuu ya shirikisho hilo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala.
Semina hiyo itashirikisha makatibu wa timu zinazotarajiwa kushiki ligi hiyo ikiwa na lengo la kuwapa maelekezo kuhusu kanuni za ligi, usajili wa timu na taratibu nyingine za ligi hiyo ikiwa ni pamoja na sheria za mpira wa miguu ambazo zimekuwa na marekebisho kwa msimu wa mwaka 2016/2017 kama zilivyotolewa na Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA

No comments