Header Ads

NAIBU Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amezitaka taasisi za fedha nchini


KALI ZOTE BLOG
NAIBU Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amezitaka taasisi za fedha nchini, kuwafikia na kuwanufaisha wakazi wengi wa vijijini na maeneo ya pembezoni ili waweze kupata fursa Naibu Spika, Dk Tulia Acksonsawa.



Dk Tulia alisema hayo katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha kisasa cha kuwahudumia wateja wakubwa, kijulikanacho kama ‘Premier Club’ cha Benki ya CRDB pamoja na Kadi mpya za Tembo Visa Infinite.
Mbali na kuipongeza benki hiyo kwa kuanzisha kituo hicho, Dk Tulia pia alisisitiza umuhimu wa taasisi za fedha, kuwafikia wananchi walioko vijijini ili nao waweze kupata fursa sawa na wale walioko mijini.
“Huduma mbalimbali za kibunifu kama hizi zinaakisi sera na azma ya Bunge pamoja na Serikali kwa ujumla ya kutaka kujumuisha wananchi wengi zaidi katika mfumo halali wa fedha,” alisema Dk Tulia.
Pia aliwataka wananchi kuondokana na tabia ya kutembea na fedha nyingi na kuhifadhi kiasi kikubwa cha fedha majumbani, badala yake wakaziweke kwenye benki ili kuepusha matukio ya kijambazi.
Akizungumzia kituo hicho pamoja na Kadi mpya ya Tembo Visa Infinite, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei alisema wameamua kuzindua huduma ya ‘Premier Club’ pamoja na kadi hiyo kwa wateja wa kundi hilo, ikiwa ni mikakati ya benki hiyo kuboresha huduma zake.
Alisema katika kituo hicho, wateja wataweza kupata huduma za kipekee ambazo zinatofautiana na wateja wa makundi mengine. Mteja atakuwa akihudumiwa na mhudumu maalumu ili kuhakikisha anahudumiwa kwa muda mfupi zaidi.
Dk Kimei alifafanua kuwa wateja waliojiunga na huduma hiyo, watapewa kadi maalumu ijulikanayo kama Tembo Visa Infinite huku wakipewa kipaumbele katika huduma mbalimbali pamoja na kupata nafuu ya tozo na riba katika huduma watakazozitumia.
Akielezea juu ya kadi hiyo mpya na ya kisasa zaidi, Mkurugenzi wa Masoko wa benki hiyo, Tully Mwambapa alisema kadi hiyo itawawezesha wateja kufurahia huduma mbalimbali za kimataifa zinazopatikana kupitia Visa, ikiwemo kupata usaidizi popote pale duniani.
“Mteja akiwa na kadi hii mpya ataweza kupata usaidizi popote pale alipo duniani kama akipotelewa na kadi yake, mteja atatumiwa kadi nyingine pale alipo pamoja na kupatiwa fedha za dharura,” alisema Mkurugenzi huyo wa Masoko

No comments