Header Ads

Sonnatah Nduka ni jina linaloanza kuwika kwenye tasnia ya filamu Tanzania

Sonnatah Nduka ni jina linaloanza kuwika kwenye tasnia ya filamu Tanzania. Pamoja na kuwa mtangazaji wa Impact Radio ya Dodoma ameonesha uwezo mkubwa kwenye uigizaji wa filamu lakini pia akiwa editor mahiri wa filamu za waigizaji wenye majina makubwa.


sonnata-nduka


sonnata-nduka
Na sasa Sonnatah anakuja na filamu aliyoigiza iitwayo ‘Kesho Yangu.’
“Kesho Yangu ni filamu ya kwanza kucheza as main actress na ndio ambayo ipo sokoni kwa sasa,” ameiambia Bongo5. “Filamu nilizowahi kucheza ni USHINDI WA MEZANI as supporting actress na “HILA HAIJENGI” nimecheza scene kama nne,” ameongeza.
Amezitaja filamu alizoshiriki kama editor kuwa ni pamoja na:
1.MZEE WA SWAGA ndani yupo JB, WASTARA, CASSIE KABWITA, THEA, na wengine..
2. CHUNGU CHA TATU ndani yumo WEMA SEPETU, JB, PATCHO MWAMBA na wengine..
3. HILA HAIJENGI ndani yupo NIVA, CHECKBUD na wengine
4. USHINDI WA MEZANI ndani yupo CHUCHU HANSI
5. KIKULACHO
6. MAHARI YA DADA
7. JINA LANGU
8. TOOL BOX
9. KESHO YANGU

sonnata


No comments