Header Ads

TRA YA SHILIKIANA NA WA FANYA BIASHALA

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema itaendelea kushirikiana na wafanyabiashara na wadau wengine kuelimisha wafanyabiashara ndogo na za kati wajisajili na kulipa kodi.

Meneja wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Gabriel Mwangosi aliyasema hayo wakati wakitoa elimu wa wajasiriamali wa kata ya Chanika wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam iliyoandaliwa kwa pamoja na Taasisi ya Jifunze Ujasiriamali Net Tanzania.

Mwangosi alisema kodi ni muhimu kwa serikali kwani hutumika kuendesha shughuli za serikali katika kutoa huduma za jamii na TRA ina wajibu wa kutoa huduma bila upendeleo na kuzingatia sheria na kanuni.

Alisema pamoja na mafanikio ya TRA, lakini bado kuna changamoto mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara kutotunza kumbukumbu za biashara sambamba na kuboresha mifumo ya ukadiriaji na ukusanyaji wa mapato ya Serikali Kuu.

Mapema akifungua semina hiyo kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’i Isaa, Mratibu Mkuu wa Masuala ya Uwezeshaji wa baraza hilo, Suleiman Malela aliipongeza taasisi hiyo na kusisitiza kwamba wametekeleza Sera ya Taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa vitendo.
Malela alisema serikali itaendelea kuhamasisha umuhimu wa kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali ili kuwezesha kukua kwa kiwango cha akiba kwa ajili ya kukopeshana na kutekeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi pamoja na za kijamii.

No comments