Header Ads

MKUTANO wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo

MKUTANO wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umemalizika mjini Mbabane nchini Swaziland na Tanzania imeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi muhimu na nyeti ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya jumuiya hiyo ambako Angola imeteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa asasi hiyo.


Image result for picha ya SAMIA HASANI

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa vyombo vya habari jana, jukumu kubwa la asasi hiyo litakuwa ni kuangalia masuala yote yanahusiana na siasa, ulinzi na usalama katika ukanda wa SADC huku changamoto kubwa ikiwa ni namna ya kutafuta suluhu ya kudumu hususan katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Lesotho.
Akizungumzia mambo muhimu yaliyojiri kwenye Mkutano huo wa 36 wa SADC, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ambaye alimwakilisha Rais John Magufuli alisema mkutano huo umekuwa wa mafanikio makubwa na amehimiza ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama katika kuwaletea wananchi maendeleo.

No comments