Header Ads

JWTZ yaadhimisha miaka 52 kwa kufanya usafi, kwata

JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeshiriki shughuli mbalimbali za kijamii wakati wa kuadhimisha miaka 52 tangu lianzishwe.

Image result for bendera ya tanzania


Miongoni mwa shughuli hizo ni usafi wa mazingira pamoja na kuchangia damu salama katika hospitali na vituo mbalimbali vya afya.
Akizungumzia shughuli zilizofanywa na jeshi hilo kwenye kambi ya Mgulani iliyopo wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam, Kaimu Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi, Basil Mrope alisema, maadhimisho hayo yalifanyika sambamba na shughuli hizo katika maeneo mbalimbali, ikiwemo kambini humo.
Pia zilifanyika shughuli za kijeshi. Kwa mujibu wa Mrope, miongoni wa shughuli za kijeshi zilizofanywa katika viwanja vya kambi ya Mgulani, Dar es Salaam ni gwaride la askari wa jeshi hilo pamoja na kurushwa kwa ndege za vita kwa mitindo mbalimbali.
“Leo (jana) tumeadhimisha miaka 52 ya jeshi letu hapa Mgulani. askari wetu wameshiriki gwaride, lakini tangu Agosti 27 tulikuwa tunafanya shughuli mbalimbali ambazo ni pamoja na usafi na kuchangia damu,” alisema Mrope.
Akizungumzia gwaride , Mkuu wa Kikosi cha Maadhimisho, Kamanda Erassy alisema kuna gwaride za aina tatu zilizofanywa na askari hao ambazo ni pamoja na kwata ya kimya kimya ambao kwa Tanzania ni mpya.
Kwa upande wake, Msemaji wa JWTZ, Ngemela Lubinga, alisema katika kuadhimisha miaka hiyo 52, wamefanya usafi na kuchangia damu katika hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
“Usafi huu ni endelevu na ni kwa nchi nzima. Tuliuanza Agosti 27 kwa kushirikiana na wananchi ,” alisema. Alieleza kuwa shughuli za Julai ni za mashujaa waliopigana vita na waliokufa kishujaa wakati za jana zilikuwa ni kwa ajili ya kuadhimisha kuanzishwa kwa jeshi hilo.

No comments