WAFUNGWA 12 KWENYE GEREZA KEKO WAACHIWA
Mchungaji wa kanisa la Mikocheni B Assemblies of God, Askofu Dr
Getrude Rwakatare, amewatoa wafungwa 12 waliokuwa wamefungwa kwenye
gereza la Keko jijini Dar es Salaam huku lengo ni kuwatoa wafungwa 78
waliofungwa kwa kukosa kulipa faini.
Mama Rwakatare akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwatoa wafungwa hao
Akizungumza na wanahabari, Askofu Rwakatare alisema kuwa amewatoa
wafungwa wanaodaiwa kiasi kidogo cha fedha na wenye makosa madogo ili
waweze kurejea uraiani na kujenga taifa kwani kuendelea kuishi huko
wanapoteza nguvu kazi ya kesho.
“Nipo gereza la Keko ambapo nina furaha kuwatoa wafungwa ambao
wamefungwa mahali hapa kwasababu mbalimbali. Wengine wameshindwa faini
ya shilingi elfu 40, wengine wameshindwa faini ya shilingi elfu 50 na
wengine kukosa faini za laki moja,” alisema. “Mimi nimeguswa kama
mtumishi wa Mungu na mchungaji wa mlima wa moto nikasema hapana
haiwezekani wacha kile ambacho tunaweza kukifanya tukifanye kwahiyo
katika gereza hili tunawatoa wafungwa 12 na tumewalipia na wamewekwa
huru, mnarudi uraiani na mimi nimewaambia kwamba wawe raia wema,
gerezani sio hoteli,” aliongeza.
“Wanaporudi wawe wananchi bora, mimi siwajui wengine wanatoka
Mkuranga, wengine Kisarawe, wengine Temeke, wengine Ilala, kama vile
tunavyoenda mahospitalini pia tuelekeze nguvu zetu magerezani kweli watu
ni wahalifu lakini wanahitaji dawa vitu vidogo vidogo kama hivi watoto
wadogo wapo pale wanahitaji dawa hata ya kikohozi. Tuje tusaidie sio
mbaya. Unamtumikia Mungu na pia nawaasa ndugu, jamaa na ninyi wake
mliorudishiwa waume zenu jamani watunzeni, watunzeni waangalieni na
muwaonye,wazee kaeni na vijana waonyeni waache mambo mabaya,kwasababu
wengine kweli wana makosa na wengine hawana makosa,wale wenye makosa
waache uovu,hawatarudi tena mahali hapa, alisisitiza.
Baada ya Keke, Mama Rwakatare ataelekea katika gereza la Ukonga kwa
ajili ya kuendelea na shughuli hiyo na amesema jumla ya kuwatoa wafungwa
hao ni shilingi milioni 25 na kwamba ameguswa yeye kama mtumishi wa
Mungu na kuwataka wanaotoka wawe wananchi bora na wakarudishe nguvu kazi
zao nyumbani.
“Tunasema turudishe nguvu kazi inayoliliwa nyumbani wakakae na wake
zao na watoto wao kwahiyo wakirudi watazalisha watafanya mambo yao,
hatutetei maovu, kurudisha pia kupunguza mlolongo wa wafungwa
magerezani.”
Post a Comment