Juhudi za uokoaji za kuwanasua watalii 45 ambao wamekwama kwenye magari ya kutumia kamba katika mlima wa Mont Blanc, Ufaransa zimeanza tena.
Juhudi za uokoaji za kuwanasua
watalii 45 ambao wamekwama kwenye magari ya kutumia kamba katika mlima
wa Mont Blanc, Ufaransa zimeanza tena.
Watalii hao walilala usiku
wa Alhamisi kwenye kibaridi kikali wakiwa wamekwama juu ya barafu
takriban 3,800m (futi 12,468) juu mlimani.
Walikuwa miongoni mwa watu 110 waliokwama baada ya magari hayo kupatwa na hitilafu Alhamisi alasiri.
Inaaminika magari hayo yalikwama baada ya kamba kushikana kutokana na upepo mkali.
Watu
65 waliokolwa kwa kutuia helikopta baadaye Alhamisi lakini juhudi
zikasitishwa giza lilipoingia na kukawa na mawingu hivyo kuifanya vigumu
kuona.
"Tulilazimika kusitisha juhudi za uokoaji kwa sababu za
kiusalama," alisema Georges Francois Leclerc, mkuu wa idara ya uokoaji
ya Haute-Savoie.
"Tunatumai tutawapata wote salama Ijumaa asubuhi," alisema ni kuongeza kwamba ni operesheni ngumu sana.
Post a Comment