Header Ads

MSAFARA wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassani ambao ulikuwa unaelekea Wilayani Tandahimba ukitokea Mtwara umepata ajali leo

MSAFARA wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassani ambao ulikuwa unaelekea Wilayani Tandahimba ukitokea Mtwara umepata ajali leo asubuhi.


 



Watu kadhaa wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea katika Kijiji cha Nanguruwe kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Majeruhi katika gari hilo ambao ni dereva pamoja na wasaidizi watatu wa Makamu Rais walipatiwa huduma ya kwanza na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mkoani humo kwa matibabu zaidi.
Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.


No comments