Header Ads

WANAKIJIJI CHA NHELEGENI KATA YA KIZUMBIbaada ya mtu asiyelikana anayesadikiwa kuwaingilia kimazingara

Wakazi wa kijiji cha Nhelegani kata ya kizumbi katika manispaa ya Shinyanga wameingiwa na hofu baada ya mtu asiyelikana  anayesadikiwa kuwaingilia kimazingara  katika nyumba zao  nyakati za usiku  na kuiba mali na kisha kuwaingilia kimwili baadhi  ya wanawake
Image result for PICHA YA MKOA WA SHINYANGA

Wakiongea na mwandishi wa KALI ZOTE BLOG  wanakijiji hao wamesema kuwa mtu huyo huingia katika nyumba za watu usiku wa manane bila wao  kutambua na kisha kuwaibia hasa simu zao za  mkononi na kisha kuwaingilia kimwili wanawake
Moja wa shuhuda  wa tukio hilo kwa masharti ya kutotajwa jina ameiambia KALI ZOTE BLOG



Image result for PICHA YA MKOA WA SHINYANGA
 unakuta umelala na mume wako cha kushangaza unamkuta mwanaume wako kalala chini au nje halafu huyo mtu anakufanyia mchezo mchafu cha kushangaza  wakati mwingine milango na madirisha tumefunga lakini ukiamka unakuta ipo wazi hakuna sehemu ilyobomolewa na  simu zimeibiwa  kama sio ushirikina nini jamani) alisema mama huyo

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la jadi sungusungu katika kijiji hicho bwana NASORO MALAJA amesema kwa sasa wanaendelea na ulinzi madhubuti na masako mkali kwa ajili ya kumbaini mtuhumiwa huyo wa wizi
Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho SENI SHIJA amekiri kupokea taarifa hizo na tayari serikali ya kijiji imekaa kikao ili kutafuta utatuzi , pia amewaomba wakazi hao kuacha kuamini katika nguvu za giza  bali usumbufu wa vibaka .


No comments