Header Ads

BABA AKATA MTOTO HOSPITALINI BAADA YA KUPEWA MTOTO WA KIKE


 Mzozo mkubwa umeibuka katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, kufuatia mwanamke mmoja aliyedai kujifungua mtoto wa kiume katika hospitali hiyo lakini muda mfupi baada ya kuruhusiwa alirudi hospitalini hapo akidai kabadilishiwa mtoto na kupewa wa kike.

 Image result for HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA
                                             COPY PICHA KWENYE MTANDAO




 Tukio hilo limetokea jana jioni baada ya mwanamke huyo Jeska Charles mkazi wa Ndala katika manispaa ya Shinyanga kurudi hospitalini hapo akiwalalamikia wauguzi wa hospitali hiyo kumpa mtoto wa kike badala ya yule wa kiume aliyejifungua,jambo ambalo lilizua mzozo mkubwa.

Baba wa mtoto huyo aliyejitabulisha kwa jina la CHARLES MATHIAS amesema mke wake alifika kujifungua katika hospitali hiyo siku ya septemba 5 mwaka huu na kulazimika ajifungue kwa njia ya upasuaji lakini  baadaye aliitwa na wauguzi na kuonyweshwa mtoto wa kiume.

Amesema baada ya kuruhusiwa hapo jana walielekezwa na muuguzi wa zamu kutomfunua mtoto huyo, lakini walipofika nyumbani walishangaa baada ya kugundua kuwa walipewa mtoto wa kike huku kadi yake  ikionyesha kuwa ni mtoto wa kiume.
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga DR.NTULI KAPOLOGWE amesema atalitolea ufafanuzi suala hilo pale atakapopata taarifa kamili.

No comments