Header Ads

shule zote za mkoa wa Shinyanga hakukuripotiwa tatizo lolote lenye kuleta picha mbaya.

Afisa elimu wa mkoa wa Shinyanga MOHAMED KAHUNDE ameeleza kuridhishwa kwake na mchakato mzima wa mtihani wa darasa la saba uliomalizika jana kote nchini, kwani katika shule zote za mkoa wa Shinyanga hakukuripotiwa tatizo lolote lenye kuleta picha mbaya.


 Image result for PICHA YA MKOA WA SHINYANGA



Bwana KAHUNDE amesema mtihani huo umeamalizika vizuri katika maeneo yote ya mkoa wa Shinyanga licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa ambazo  ni pamoja na wanafunzi wachache kutoweza kufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba,utoro,vifo,ugonjwa na migogoro ya kifamilia.
Amesema hivi sasa ofisi yake inasubiri taarifa kutoka katika maeneo mbalimbali ili kufahamu idadi kamili ya wanafunzi walioshindwa kufanya mtihani huo.

Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka huu ulikuwa na watahiniwa wapatao 25 elfu na 531 ambao wanatoka katika jumla ya shule za msingi 567,huku 24 kati yake zikiwa ni za mchepuo wa kiingereza

No comments