Mwakyembe: Rais Magufuli hajavunja sheria
KALI ZOTE BLOG
BUNGE limeelezwa kuwa Rais John Magufuli hajavunja sheria yoyote kwa
kuzuia siasa za hovyo, iliyotafsiriwa kuwa amefuta siasa nchini, bali
kwa kufanya hivyo ameiheshimu, ameihifadhi na kuilinda Katiba ya nchi.
Aidha, wanasiasa na watu wengine wanaodhani Rais amevunja sheria, wameshauriwa kwenda mahakamani au kudai majadiliano na Rais.
Hayo yalisemwa juzi jioni mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria,
Dk Harrison Mwakyembe alipokuwa anahitimisha mjadala wa Muswada wa
Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa wa Mwaka 2016, aliouwasilisha bungeni
na kujadiliwa kwa siku mbili mfululizo.
Mwakyembe alilazimika kuyasema hayo baada ya wabunge wa kambi ya
upinzani, kuwashambulia waziri huyo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
George Masaju kuwa hawaungi mkono muswada uliowasilishwa bungeni kwa
kuwa una nia ovu.
“Dk Mwakyembe huyu huyu ndiye aliyetetea kauli ya Rais Magufuli ya
kuzuia mikutano ya hadhara wakati anajua inakubalika kikatiba,” alisema
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema aliyeungwa mkono na Mbunge wa
Momba, David Silinde na Mchungaji Peter Msigwa wa Iringa, wote wa
Chadema.
Akijibu, Dk Mwakyembe alisema ni vyema wakaacha kuingilia utendaji wa
Rais Magufuli na wasaidizi wake, kwani hawana mamlaka hiyo na kwamba
kama wanadhani wanao
newa, wana njia ya kutafuta haki kupitia Mahakama
.
“Mimi sikujua mkuki kwa nguruwe binadamu mchungu, jana mliongea
nikawasikiliza tulieni na mimi leo niwaeleze na nijibu hoja zenu,”
alisema na kuongeza kuwa hawezi kubishana nao kwani anatilia mashaka
usafi wao katika siasa, kwani walizunguka nchi nzima kumtangaza Edward
Lowassa kuwa ni fisadi, lakini alipohamia kwao akageuka `malaika’
wanayemlamba nyayo zake.
Baada ya kauli hizo, alisisitiza Rais Magufuli hajavunja, sheria wala
Katiba katika kupeleka muswada huo, bali alichokifanya ni kuzuia siasa
za shari zisisambaratishe taifa.
Waziri huyo alisema alitegemea busara ya chama chochote kwenda
mahakamani au kufanya majadiliano na serikali, Mwanasheria Mkuu au
waziri mhusika, lakini hakuna mtu yeyote aliyekwenda mpaka Muswada huo
unaletwa bungeni kupitishwa.
Kauli kama ya Mwakyembe ilitolewa pia na Mwanasheria Mkuu, George
Masaju aliyehoji ni kifungu gani cha Katiba kilichokiukwa na Rais na
kutaka wanaoamini wako sahihi, ni vyema wakafuata mkondo wa Sheria na
kwenda kushitaki mahakaman
Post a Comment