KENYA YA RUHUSU WA SICHANA WA KIISLAM KUVAA JUBA
Wasichana wa kiislam wanaosoma shule nchini Kenya wanapaswa 
kuruhusiwa kuvaa  hijab kama sehemu ya sare zao za shule , imeamuru 
mahakama ya rufaa. 
Uamuzi huo wa kihistoria uliotolewa na majaji
 watatu umekuja baada ya kanisa la kimethodist kupinga muongozo kutoka 
kwa mamlaka za nchi hiyo kuwaruhusu wasichana wa shule wa kiislamu kuvaa
 hijab ama vilemba katika shule yake.
 Wanafunzi wa kiislam katika
 shule ya sekondari ya St Paul Kiwanjani School  kaunti ya  Isiolo  
walipigwa marufuku kuvaa hijab na suluari nyeupe pamoja na sare ya 
shule. 
Kanisa hilo lilidai kuwa uamuzi wa kuwaruhusu wanafunzi 
wasichana  wa kiislamu  kuvaa  mavazi tofauti umesababisha  uhasama 
miongoni mwa wanafunzi.
Mahakama ya juu iliunga mkono kanisa na kusema kuwa wasichana hawawezi kuvaa hijkabu shuleni.
Lakini
 majaji katika mahakama ya rufaa wamesema kuwa ni jukumu la wanaotoa 
elimu  kukubali maadili na kanuni za utu, na za matabaka mbali mbali ya 
watu, na bila ubaguzi , limeripoti  gazeti la Star nchini Kenya.
Kwa
 mujibu wa gazeti la  East African Standard, majaji hao waliongeza 
kusema kuwa vazi la kidini haliwezi kulinganishwa na mtindo wa vazi 
unaokwenda na wakati  
Shule za kitaifa huruhusu wasichana kuvaa hijab.
Post a Comment