Header Ads

Paul Makonda ameingia kwenye awamu anayoiita ni ya pili kwa kutaja orodha ya watu ambao watahitajika kufika Polisi Central Dar es salaam

Leo February 8, 2017 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameingia kwenye awamu anayoiita ni ya pili kwa kutaja orodha ya watu ambao watahitajika kufika Polisi Central Dar es salaam kusaidia taarifa na maelezo kwenye mapambano ya kutokomeza dawa za kulevya Dsm.
Kwenye orodha hiyo iliyosambaa mitandaoni kwenye jina namba 54 kuliandikwa Philemoni Mbowe na hivyo habari zikaanza kusambaa kwamba sio Freeman Mbowe aliyetajwa.
Jioni hii Paul Makonda amewaambiwa Waandishi wa habari kwamba jina la kwanza kwenye namba 54 lilikosewa na inatakiwa kuandikwa Freeman Mbowe hivyo anaehitajika Ijumaa ni Mheshimiwa Freeman Mbowe.
VIDEORC Makonda akitaja orodha ya awamu ya pili, tazama kwenye hii video hapa chini


No comments