Model wa muda mrefu toka Tanzania Daxx Cruz Model amefunguka na kusema yeye anamkubali zaidi Diamond Platnumz zaidi kuliko Alikiba kutokana na ukweli kwamba Diamond Platnumz hata ukimbeba anabebeka ila siyo Alikiba.
Daxx Cruz amesema hayo alipokuwa kwenye kipengele cha KIKAANGONI kinachofanyika kila siku ya Jumatano kwenye ukurasa wa Facebook wa EATV
"Mimi namkubali zaidi Diamond Platnumz kuliko Alikiba kwa kuwa ni mtu ambaye ukimshika mkono anakufuata, lakini hata muziki wao pia uko tofauti" alisema Daxx Cruz
Mbali na hilo Daxx pia alimuelezea msanii Jux na kusema ni kati ya wasanii ambao kwanza anajitambua na kufanya vizuri lakini pia wanamuonekano mzuri na vitu vyake vipo kwenye mpangilio.
Daxx Kikaangoni
"Kati ya Ben Pol na Jux mimi namkubali sana Jux, kwa sababu Jux yupo vizuri katika kila sekta, muonekano, kimuziki, hata mpangalio wa mavazi yake nje ya muziki, stejini hata kwenye video zake. Maana wapo wasanii wengine wanavyovaa kwenye video ndiyo wanavaa hivyo mtaani" alisema Daxx Cruz
Daxx pia aligusia suala la yeye kuwasaidia ma-model wa Tanzania na kusema kwa sasa hayupo tayari kumsaidia mtu yeyote ila wanatakiwa kupambana na kupigania ndoto zao wao wenyewe, yeye anaweza kuwapa njia za kupita kufikia malengo yao.
"Mimi sina mpango wowote kuinua modeling ya Tanzania, kila mtu ahangaike kivyake saizi mimi namfikiri Daxx na Linda tu, sina mpango huo kwa sasa kiukweli ila mtu akinifuata naweza kumpa njia ya kupita tu" alisema Daxx
Post a Comment