Viongozi wa Dini Mkoani Shinyanga, wamepongezwa
Viongozi wa Dini Mkoani
Shinyanga, wamepongezwa kwa kushirikiana na serikali katika shughuli mbalimbali
za kitaifa, kwani wamekuwa kiungo muhimu
na mchango mkubwa katika Maendeleo na ujenzi wa Taifa la Tanzania.
Naibu msajili wa
Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga SEKELA MWAISEJE ameyasema hayo Jana kwenye kilele cha wiki ya
sheria nchini,kwamba viongozi wa dini wamekuwa na ushirikiano wa dhati katika
shughuli mbali mbali za kitaifa
MWAISEJE amesema
mchango wa viongozi wa dini katika
maendeleo ya Taifa unapaswa
kuthaminiwa na kuheshimiwa.
Katika maadhimisho
ya wiki ya Sheria nchini katika viwanja vya Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya
Shinyanga,viongozi wa dini kutoka madhehebu mbali mbali walihudhuria ambapo Kabla
ya kuanza kwa shughuli hiyo,viongozi hao
walitoa sala na dua kwa lengo la kuiombea idara ya mahakama,wadau wa
sheria,nchi, na viongozi wa serikali.
Katika taarifa
yake Jaji mfawidhi mahakama kuu kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga mheshimiwa
RICHARD KIBELA amewataka mahakimu kutumia adhabu mbadala katika baadhi ya kesi ili
watuhumiwa waweze kuwa nje wakiendelea na shughuli za kukuza uchumi,badala ya
hukumu ya kifungo gerezani.
Post a Comment