Yanga yawafuata Wacomoro
Kikosi cha wachezaji 20 cha Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara Yanga kinaondoka leo jumamosielekea nchini Comoro kwa ajili ya mchezo wake wa Kwanza wa Klabu bingwa Afrika dhidi ya mabingwa wa nchini hiyo Ngaya
Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Yanga SC kinatarajiwa kuondoka alfajiri ya kesho kuelekea nchini Comoro kwenye mji wa Moroni tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Jumapili ya Februari 12 mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kumaliza mazoezi Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema, wanahitaji kuondoka na pointi tatu mbele ya mabingwa hao wa Comoro ambao wamepata taarifa zao pekee na hawakuwahi kuwaona lakini wamejipanga kwa kutumia taarifa chache walizozipata.
Mwambusi amesema, kikosi kipo kamili kwa ajili ya kupambana isipokuwa baadhi ya wachezaji watabaki kutokana na matatizo mbalimbali kama Mshambuliaji Donald Ngoma ambaye ni majeruhi pamoja an beki Andrew Vicenti Dante ambaye anaadhabu ya kadi nyekundu aliyoipata katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika katika hatua ya makundi dhidi ya TP Mazembe ya nchini Congo.
Donald Ngoma
Kwaupande wake Nahodha wa Yanga Nadir Haroub Canavaro amesema, watahakikisha kila mchezaji anatumia nafasi yake katika mchezo huo ili kujihakikishia wanaibuka na pointi tatu ambazo zitawasaidia katika mchezo wa marudiano na hatimaye kuweza kusonga mbele zaidi katika michuano hiyo.
Canavaro
Msafara utakuwa na wachezaji ishirini (20) benchi la ufundi nane ( 8 ) pamoja na viongozi wawili (2).
Wachezaji wanaoondoka kesho ni.
Deogratius Munish, Ally Mustafa, Deud Kaseke, Haruna Niyonzima, Thaban Kamusoko, Amissi Tambwe, Mwinyi Haji, Saimon Msuva, Geoffrey Mwashuiya, Saidi Makapu, Hassan Ramadhani, Juma Mahadhi, Yusuph Mhilu, Obrey chirwa, Nadir Haroub, Justine Zulu, Kelvin Yondani, Juma Abdul, Oscar Joshua na Emmanuel Martin.
Benchi la ufundi wanaoondoka ni:
George Lwandamina, Noel Mwandila, Edward Samwel Bavu, Juma Pondamali, Juma Zakaria Omary, Hafidhi Saleh Suleiman, Mohamed Omary Mwaliga na Jacob Sospeter Onyango.
Viongozi wanaosafiri.
Mussa Mohamed Kisoki (TFF) na Paul Malume (Yanga Sc)
Baada ya kikosi kuwasili kinatarajiwa kufanya mazoezi yake kesho jioni kwenye uwanja utakaochezewa mchezo siku ya Jumapili.
Post a Comment