Header Ads

Kabanza atambulisha Ngoma yake ya Digital alichomshirikisha Ydee



Msanii  chipukizi wa Kizazi kipya Bongo flava Kabanza kutoka jijini Mwanza, ametambulisha leo kibao chake kipya kiitwacho Digital alichomshirikisha Ydee kilichotengenezwa na  Adolf Beatz pamoja na  producer Doucher Master.


Kabanza itakuwa Track yake ya tatu baada ya kibao chake cha kwanza kilichomtambulisha kiitwacho  Money na cha pili Mdananda alichokifanya mwaka jana akishirikiana na Ydee ambacho kilikuwa hit kwenye media za jijini hapa kutokana na Ujumbe, uliokuwemo, Melody na Beatz 


Msanii huyo mwenye jina lake halisi  Kabanza Peter ambaye ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma anayechukua Degree ya Chemistry, alipenda mziki toka anasoma shule ya msingi na kujiingiza kwenye vikundi vya sanaa shuleni alipokuwa O’level pia na kufanya vizuri Shule ya Sekondari Bugogwa iliopo Ilemela jijini Mwanza.

Aidha aliomba watanzania wapenda mziki wa kizazi kipya bongo flava kumpa sapoti kadri wawezavyo ili kumfikisha sehemu anayostahili.

“Nimeachia Kibao changu kipya leo  February  2, 2017 kiitwacho Digital nilichomshirikisha Ydee, naomba washabiki na wapenda mziki wa kizazi kipya wakipokee wasikilize na pia naomba wadau wanisapoti ili nifike mbele zaidi,” alisema Kabanza.

Kwa upande wake Msanii huyo  anaamini heshima na nidhamu ndio nguzo bora katika kufanya vizuri na kupaa juu zaidi.

imeandikwa na mwandishi wetu  wa KALI ZOTE BLOG  ames Timber kutoka 


No comments