JIPYA: Ni kuhusu yule Mjanelijitokeza mbele ya Rais Magufuli na kusema amedhulumiwa mali za mume wake huko Tanga
Wiki iliyopita Mwanamke aitwae Swabaha Mohamed alijitokeza mbele ya Rais Magufuli na kusema amedhulumiwa mali za mume wake huko Tanga na pamoja na kudhulumiwa amekua akitishiwa maisha.
AzamTV imefika nyumbani kwa Mke mkubwa wa Marehemu Shosi huko Tanga ambaye amesema amesikitishwa na kitendo cha Swabaha kujitokeza mbele ya Rais Magufuli akidai alikua Mke pekee wa marehemu Shosi.
Mariam ambaye ni Mke mkubwa wa Marehemu Shosi amesema >>> “Marehemu Mzee Mohamed Shosi alikua na Wake watatu, mimi nikiwa mke wa kwanza kabisa alinioa wote tukiwa wadogo na tukapata watoto 7, akaja akaoa mke mwingine akazaa nae watoto watatu lakini akafariki kwa ajali ya gari”
“Baadae akaoa Mke mdogo na kuzaa nae mtoto mmoja, tumeshangazwa sana na Swabaha ametudhalilisha sana na kusema Mwanangu anauza unga, hiyo sio kweli ni uongo kabisa… tunakuomba Mh. Rais utume tume yako waje kutuchunguza na sisi”
Mariam amedai kwamba Swabaha alikua anamuita Marehemu Mjomba na anae Mume wake halali ambaye anaishi Tanga, sio mjane… ana mume na ni Wakili anaefanya kazi Tanga……. tazama kwenye hii video hapa chini kupata taarifa kamili
Post a Comment