Header Ads

Bingwa wa dhahabu kwenye mashindano ya London 2012, Mariya Savinova wa Urusi, avuliwa taji lake


Mariya Savinova alinyakuwa dhahabu katika mbio za Dunia za mita 800 mwaka 2011, Korea Kusini

Bingwa wa dhahabu kwenye mashindano ya London 2012, Mariya Savinova wa Urusi, avuliwa taji lake
Mshindi wa nishani ya dhahabu mwaka 2012 katika mbio za mita 800 za huko London Mariya Savinova, amevulia taji lake na kupigwa marufuku kushiriki mashindano yoyote ya mbio hadi mwaka 2019.
Matokeo yote ya mbio za mwanariadha huyo tangu Julai 10, 2010 hadi Agosti 2013, zimefutiliwa mbali, baada ya kupatikana ametubia dawa za kusisimua misuli.
Savinova alimpiku Caster Semenya wa Afrika Kusini katika mashindano hayo ya Olimpiki Jijini London na pia mbio za dunia za riadha mwaka 2011 huko Daegu, Korea Kusini.Mkimbiaji huyo mwenye umri wa miaka 31 pia alimshinda Muingereza Jenny Meadows katika mbio za mataifa ya Bara Ulaya mwaka 2010 na kumfanya kunyakua medali ya shaba. Sasa medali zote za wanariadha hao wawili Jenny Meadows na Caster Semenya zitaboreshwa.
Savinova pia atapoteza dhahabu yake katika mbio za mita 800 ya mwaka 2011 pale aliposhinda mashindano ya mataifa bingwa barani Ulaya.
Taarifa kutoka katika mahakama inayosikiza makosa ya kimichezo: "Kwa misingi ya ushahidi tosha, ikijumuisha pia ushahidi kutoka kwa hati ya kuzaliwa (ABP), Mariya Savinova amepatikana akijihusisha na utumiaji wa dawa za kusisimua misuli tangu Julai 26, 2010 (Usiku wa kuamkia mashindano ya mataifa bingwa Ulaya yaliyokuwa yakifanyikia mji wa Barcelona) muda wote hadi Agosti 19, 2013 (siku ya mashindano ya dunia Jijini Moscow).
Savinova ni miongoni mwa wanariadha watano wa Urusi waliotajwa katika ripoti ya na mamlaka kuu ya kukabiliana na dawa za kusisimua misuli miongoni mwa wanariadha (WADA).
Hajashiriki mbio tangu mwaka 2013 pale aliposimamishwa ili achunguzwe baada ya video kuhusu matumizi ya madawa hayo kufichuliwa na mpekuzi Yuliya Stepanova.

No comments